×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WAZIRI MKUU ASHIRIKI SWALA YA EID, RUANGWA

Na Mwandishi wetu.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 31, 2025 amejumuika na waumini wa dini ya kiislam katika Swala ya Eid iliyofanyika kiwilaya kwenye Mtaa wa Maghalani, Ruangwa Mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya swala hiyo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa waumini hao na Watanzania kwa ujumla kuliombea Taifa, viongozi wake pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano.

Katika Swala hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alishiriki.

#NTTupdates