×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA MAAFISA WATENDAJI WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi wetu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Siku mbili wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Africa ulioanza leo Mei 12, 2025, katika ukumbi wa Hotel ya Sofitel jijini Abidjan nchini Ivory Coast. Mheshimiwa Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo.

Mkutano huo ambao umefunguliwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara umewakutanisha Maafisa Watendaji Wakuu zaidi ya 2,000, wawekezaji na Wakuu wa Nchi na Serikali.

#NTTUpdates