×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WENYE UWANJA WAMEWAITA JE KITAPIGWA ?

Na Mwandishi wetu.

Baada ya muendelezo wa mtifuano kati ya bodi ya ligi kuu TPLB na klabu ya Young Africans SC na kuleta mashaka kuwa huenda derby namba 3 kwa ubora Afrika, kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya Wananchi Young Africans SC, isichezwe kwenye mzunguko wa pili, Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa, Habari na Michezo imeamua kuingilia kati swala hilo ili kupata suluhu.

Waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi amekutana viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) Klabu ya Yanga SC na Simba SC ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara maarufu kama Kariakoo Derby.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika leo jijini Dar es Salaam, Machi 27 kitaongozwa na Waziri Kabudi.

Kariakoo Derb ilighairishwa na Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) siku ya Jumamosi Machi 8, 2025 saa chache kabla mchezo kuanza huku sababu ikitajwa kuwa basi lililobeba wachezaji wa Simba SC kwa ajili ya mazoezi ya mwisho siku ya Ijumaa Machi 7, 2025 lilizuiwa kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kwenda uwanjani bila kutoa taarifa kwa wenye mamlaka ya uwanja na timu mwenyeji kwenye mchezo huo na kupeleka Simba SC kutangaza kutocheza mchezo huo.

#NTTupdates