ร—
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WIZARA YA MICHEZO KUVUNA HELA KUPITIA (BETTING)

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

SERIKALI imeeleza kuwa ipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau wa michezo kuihamisha bodi ya michezo ya kubashiri (Betting) kutoka Wizara ya Fedha kwenda Wizara ya Michezo ili kuinufaisha sekta ya michezo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Juni 6,2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Shabani Hamisi Taletale mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambaye aliuliza Serikali haioni haja ya kuihamisha michezo ya kubahatisha kutoka Wizara ya Fedha kwenda wizara ya Michezo kutokana na michezo hiyo kunufaisha asilimia 5 kwenye sekta hiyo kutokana na kusimamiwa na Wizara ya Fedha.

Waziri Majaliwa amesema bodi ya michezo ya kubahatisha iko Wizara ya Fedha na anayekusanya mapato ni TRA kama vile kodi zingine zinavyokusanywa na TRA na baada ya kukusanya fedha baraza la michezo lililoko ndani ya Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo linapata asilimia tano ya mgao wa makusanyo ya fedha kutoka katika michezo hiyo.

#NttUpdates