Na Mwandishi wetu.
MABINGWA wa kihistoria ligi kuu Tanzania Young Africans SC wametangaza tarehe 4/8/2024 kuwa kilele cha wiki ya mwananchi kuelekea msimu ujao.
Tamasha hilo hutumika kumtambulisha kikosi kitakachotumika na klabu hiyo kuelekea msimu ujao.
Ni utamaduni wa vilabu kadhaa Tanzania bara kuwa na matamasha maalumu ambayo hutumiwa kutambulisha wachezaji wapya na kuhitimishwa kwa kucheza mchezo wa kirafiki.
#NTTUpdates