Na Mwandishi wetu.
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans SC wameondoka rasmi leo mchana kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kambi kuelekea msimu ujao na mialiko miwili waliyoipata kutoka kwenye vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Afrika Kusini.
Young Africans SC itacheza dhidi ya Augsburg inayoshiriki ligi kuu Ujerumani (Bundesliga) tarehe 20/7/2024 siku ya jumamosi kwenye mashindano ya Mpumalanga International premier Cup 2024, pia tarehe 28/7/2024 itacheza dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye mashindano ya Toyota Cup 2024.
#NTTupdates