Na Mwandishi wetu.
Baada ya klabu ya Young Africans SC kuitikia wito kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF) juu ya sakata lao la kudai fedha zao za zawadi ya mshindi wa kombe la CRDB msimu uliopita, ambapo shirikisho hilo likitoa taarifa rasmi kwa umma kuwa klabu hiyo ndiyo inadaiwa fedha na kuwataka wafike ofisini kwao Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Leo Juni 11,2025 ili kuhakiki madeni yao.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho kati ya TFF na Young Africans SC, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine ameweka wazi kuwa wao wanachotaka ni fedha zao tu na si jambo jingine”.
“Kitu pekee tulichowaambia ni tunataka fedha zetu za ubingwa, hatutacheza mchezo wowote hadi pale tutakapolipwa pesa zetu”
Sakata hilo limeendelea kuibua maswali mengi kwa wadau wa soka nchini Tanzania juu Maendeleo ya soka kwa ujumla.
#NTTupdates