×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

YANGA SC “TUPENI ALAMA ZETU TATU NA HATUNA IMANI NA KAMATI”

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Young Africans SC kupitia Kamati ya Utendaji chini ya Rais wa klabu hiyo Eng. Hersi Said, imefanya Kikao cha dharura hapo jana March 9, 2025 kwa njia ya mtandao ambapo wametoa msimamo wao kutaka wapewe haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi.

Kadhalika imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 dhidi ya Simba SC kwa tarehe yoyote itakayopangwa na bodi ya ligi kuu (TPBL)Klabu hiyo imesema kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu hiyo imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo imeliomba Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuivunja kamati hiyo na kuteua Viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.

Pia imewaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa klabu ya Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendele.

#NTTupdates