Na Mwandishi wetu.
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania bara, Young Africans SC imeendelea kupanda thamani na inakadiriwa kufikia Bilioni 100 kutokana na kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza kwenye klabu hiyo yamesenwa na Mwenyekiti wa Kamati ya mabadiliko wa klabu hiyo Wakili Alex Mgongolwa kupitia mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Septemba 7, 2025 katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki Dar es Salaam.
“Baada ya tathmini ya kina klabu ya Yanga SC imefikia thamani ya Shilingi Bilioni 100”.
Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kuelekea msimu mpya ambao wanachama na wadau mbalimbali wanahudhuria ili kujua dira ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya.
#Yangasc
#NTTupdates