×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

YANGA SC YAIWEKA KIKAANGONI BODI YA LIGI

Na Mwandishi wetu.

Hali si shwari kwa Viongozi wa bodi ya ligi kuu baada ya Uongozi wa klabu ya Young Africans SC kuendelea na msimamo wao wa kutochezo mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya mahasimu wao Simba SC mpaka pale bodi ya ligi (TPLB) itimize matakwa ya klabu hiyo ambayo wameyawasilisha kwa njia ya maandishi.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi na klabu ya Young Africans SC kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ikiweka wazi msimamo wao juu ya mchezo huo ambao awali ulipangwa kucheza Machi 8, 2025 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam lakini bodi ya ligi ilighairisha mchezo huo saa chache baadae.

Miongoni mwa matakwa ya Young Africans SC ni kujiuzulu kwa baadhi ya Viongozi wa bodi ya ligi na TFF kutokana na kushindwa kusimamia kanuni ambazo zinawaongoza kwenye majukumu yao.

#NTTupdates