Na Mwandishi wetu.
Uongozi wa klabu ya Young Africans SC leo Juni 30, 2025, imepeleka makombe yote matano ambayo wameshinda msimu huu kwenye mashindano mbalimbali kwa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi.
Pia klabu hiyo ilimzawadia Rais Dkt. Hussein Mwinyi medali ya ubingwa wa kombe la CRDB walilotwaa hapo jana baada ya kuifunga klabu ya Singida Black Stars kwa magoli 2-0 kwenye dimba la New Amaan Complex pamoja na jezi ya Yanga Bingwa.
Pia serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeipongeza klabu hiyo kwa kutwaa mataji hayo na kuendelea kuitangaza Zanzibar hasa kwenye sekta ya utalii.
Young Africans SC inakuwa timu ya kwanza kupeleka Makombe matano ndani ya msimu mmoja Ikulu Visiwani Zanzibar.
#NTTupdates