×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ZAMALEK SC WAMTIMUA JOSE PESEIRO

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Zamalek SC ya Misri imemfuta kazi Kocha wao Jose Vitor dos Santos Peseiro (65), raia wa Ureno baada ya muendelezo wa matokeo yasiyoridhisha ambayo wamekuwa wakiyapata msimu huu kwenye mashindano mbalimbali.

Zamalek iliondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) na klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini lakini pia imepoteza matumaini ya kubeba taji la ligi kuu nchini Misri (Nile premier League) msimu huu licha ya kuwa nafasi ya 3 kwenye msimamo huku wakitoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa jana dhidi ya National Bank.

Peseiro ambaye alijiunga na Zamalek SC Februari 2025 ameiongoza klabu hiyo kwenye michezo 17 akishinda michezo 8, sare 7 na vipigo 2 kwenye mashindano mbalimbali ambayo wameshiriki.

#NTTupdates