Na Mwandishi wetu.
Tatizo la Majeraha kwa nyota wa timu za Taifa Ulaya imekuwa jambo lae kawaida hasa kipindi hichi ambacho mastaa hao wameenda kutumikia timu zao za Taifa kwa ajili ya kufuzu michuano ya kombe la Dunia mwaka 2026.1.
Riccardo Calafiori (22) ameondoka kambini Italia mara moja baada ya kuumia goti huku madaktari wa timu ya Taifa ya waliweka wazi kuwa tathmini ya mwisho itafanywa na wataalam wa Arsenal.2.
Ryan Gravenberch (22), ameondoka kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Uholanzi (The Oranges) na kurejea Liverpool ili kufanyiwa vipimo zaidi kujua ukubwa wa jeraha lake, kiungo huyo muhimu kwenye klabu hiyo.3.
Lionel Messi (37) Nahodha wa Argentina na klabu ya Inter Miami nchini Marekani pia anakosekana kwenye michezo ya kufuzu kombe la Dunia 2026 baada ya kupata majeraha ya misuli.4.
Pau Curbasi (17) mlinzi wa kati wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania pia ameondolewa kwenye kambi ya timu ya Taifa baada ya kupata majeraha.5.
Neymar Jr (33), winga wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Santos majeraha yamemfanya nyota huyo kujiondoa kwenye kikosi ili aweze kupona na kurejea timamu kwenye kikosi Cha Brazil.
#NTTupdates.