×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ZOEZI LA MSAADA WA KISHERIA NI ENDELEVU -DKT. NDUMBARO

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amewatoa wasiwasi wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na Watanzania kwa ujumla waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia ( Mama Samia Legal Aid Campaign) kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na sio la mwezi mmoja ambapo Serikali imeandaa na kuanzisha madawati ya msaada wa kisheria katika kila Halmashauri hapa nchini ambapo wataalamu wa sheria watakuwa wakitoa huduma hiyo na elimu kwa wananchi kila wakati.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo leo Machi 28, 2025 Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya msaada wa kisheria kwenye uwanja wa Ngarenaro Jijini humo ambapo ameeleza mnama ambayo Wizara hiyo ya Katiba na Sheria imejipanga vyema kuhakikisha Watanzania wanapatiwa huduma hiyo.

Aidha, Ndumbaro amezitaka ofisi zote za kisheria na vyombo vingine vya kisheria ndani ya mkoa huo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha wanawahamasisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi ndani ya muda huo wa siku kumi (10) uliopangwa kwaajili ya kutatua kero na changamoto zinazohitaji msaada wa kisheria.

#NTTupdates.