Na Mwandishi wetu.
Saa chache zimesalia kushuhudia mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Wananchi Young Africans SC dhidi ya Mnyama Simba SC maaarufu kama Kariakoo derby katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam majira ya saa 10:00 Jioni.
Young Africans SC ndiye mwenyeji wa mchezo huo ambapo anashikilia rekodi ya kumfunga mtani wake Simba SC mara 5 mfululizo huku Simba SC ikijinadi kuwa itapata ushindi wake wa kwanza leo na kuondoa uteja wake kwa Wananchi.
#Ngaoyajamii
#NTTupdates