Na Mwandishi.
Mjumbe wa Halmashauri ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa, Chacha Wambura ameibuka na ushindi wa kura za maoni kwa kuapata ya jumla ya kura 2145 akimshinda Constantine Kanyasu Mbunge aliyemaliza muda wake kwa kupata kura 2097.
Jumla ya wajumbe halali walioshiriki kupiga kura katika jimbo la Geita mjini walikuwa 5682 ambapo watia nia wengine walikokuwa katika kinyang’anyiro hichoni ni pamoja na Mwl.
Saulo (34) Eng. Robert Gabriel (119), Upendo Peneza (1272).Wilaya ya Geita yeye majimbo 4 kumeshuhudiwa Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Busanda kwa miaka mitano safari hii ameshindwa kuchomoza kwenye kura za maoni katika jimbo Jipya la Katoro ambapo ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 1265, Kija Ntemi ameongoza kura (2134), akifuatiwa na Ester James (2075), Simoni Marando (549) na Mathias Lupuga (232).
Jimbo la Busanda Dkt. Jafary Seif ameibuka mshindi kwa kupata jumla ya kura 5286 akifuatiwa na Lorencia Bukwimba (927) Dkt. Busanda Lucas (392) na Dkt. Salum Mathias (23).
Na katika Jimbo la Geita Mbunge aliyemaliza muda wake Joseph Kasheku maarufu Musukuma ameibuka mshindi kwenye kura hizo za maoni kwa kupata kura 5251 waliomfuata ni Emmanuel Luponya (1,997), Patrick Stephen (381) na Sophia Mashala (44).
#NTTupdates.