Na Mwandishi wetu.
Mabingwa mara nne mfululizo wa ligi kuu ya NBC Young Africans SC, imemtambulisha kiungo wao mpya Mohamed Doumbia raia wa Burkina Faso akitokea Majestic FC.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akitajwa na vilabu kadhaa vikihitaji huduma yake kutokana na kuhimili vyema eneo la kati la uwanja.
Doumbia ambaye aliwahi pia kupita vilabu vya Ekanas IF ya Poland, FK Dukla Prague na Fe Slovan Liberec za Jamhuri ya Czech anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaotoa mchango mkubwa kwa Yanga SC msimu ujao kutokana na uwezo wake dimbani.
#NTTupdates