×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

HUYNH ATWAA TAJI LA MISS INTERNATIONAL 2024

Na Mwandishi wetu.

Mlimbwende Huynh Thi Thanh Thuy (22) ameingia kwenye rekodi ya kuwa Miss wa kwanza kutokea nchini Vietnam kushinda taji la Miss International 2024 akiwashinda warembo wengine kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

Mashindano hayo yamefanyika Tokyo Dome City Mall, Tokyo nchini Japan ambapo mrembo huyo aliwashinda walimbwende wengine 70 kutoka mataifa mbalimbali.

Aliposikia jina lake likitajwa kama mshindi Huynh alizidiwa na hisia kali na kulia wakati Miss International 2023 Andrea Rubio raia wa Venezuela akiweka taji juu ya kichwa cha mrembo huyo huku shangwe kutoka kwa watazamaji waliohudhuria tukio hilo.

“Mimi ni Miss Vietnam wa kwanza kuja Miss International na sasa mimi ni Miss International wa kwanza kutoka Vietnam,” “naweza kuthibitisha kwamba ninastahili upendo na usaidizi kutoka kwa watazamaji wangu kutoka Vietnam na duniani kote, Asante sana.”

Miss Huynh Thi Thanh Thuy aliyasema hayo baada ya kuvikwa taji hilo la Miss International 2024.

#NTTupdates