Na Mwandishi wetu
Msanii wa Bongo Fleva Marioo, ameibuka kidedea baada ya kutwaa tuzo ya mwimbaji bora wa mwaka kwenye tuzo za Muziki Tanzania ( TMA) zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Superdome Masaki Dar es Salaam.
Marioo ameahinda tuzo hiyo akiwashinda wasanii wenzie ambao ni1. Harmonize 2. Diamond Platnumz 3. Alikiba na 4. Jay Melody.
Marioo alikabidhiwa tuzo yake na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma “Mwana FA”
#NTTupdates