×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MSUVA SAMATTA WATEMWA TAIFA STARS JOB ARUDISHWA

Na Mwandishi wetu.

Kocha wa Taifa stars Hemedi Seleman, amemjumuisha mlinzi wa kati wa Young Africans SC Dickson Job kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakao ingia kambini kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu michuano ya Afcon 2025 nchini Morocco.

Nyota huyo ambaye alikuwa na mgogoro na Kocha Hemedi Seleman na kupelekea kuachwa mara kadhaa kwenye timu ya Taifa licha ya kufanya vizuri kwenye klabu yake ya young Africans SC, kwenye michuano ya kimataifa.

Pia washambuliaji wawili Mbwana Samatta na Simon Msuva, hawajajumuishwa kwenye kikosi hicho kitakachoingia kambini kujiandaa dhidi ya Guinea na Ethiopia.

#NTTupdates