Na Mwandishi wetu.
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya kadi za malipo ya MASTERCARD wamezindua suluhisho jipya la malipo na la kwanza duniani, lijulikanalo kwa jila la NMB QR PAY BY LINK, ambapo kupitia suluhisho hilo mteja yeyote yule duniani mwenye kadi ya VISA, MASTER CARD NA UNION PAY, atakuwa na uwezo wa kufanya malipo popote pale duniani kwa kutumia simu yake ya mkonini.
Aidha Suluhisho hilo la malipo la NMB QR PAY BY LINK, mfanyabiashara wa hapa nchini anachotakiwa ni kutembelea tawi lolote la benki ya NMB kujisajili na huduma hiyo ni bure kwao, huku mteja anachotakiwa ni kujisajiri mara moja kwenye mfumo wa PAY BY LINK baada ya hapo atakachokuwa anatakiwa kufanya ni kuscan kwa kutumia simu yake ya mkononi kufanya manunuzi bila kuangalia ni aina gani ya kadi anayotumia.
Akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa suluhisho hilo la malipo lijulkanalo kwa jina la NMB QR PAY BY LINK, uzinduzi uliofanyika kisiwani Zanzibar, Katibu Mkuu wizara ya Utalii na mambo ya kale Zanzibar Dkt. Aboud Suleiman Jumbe, amesema kwa mwaka huu pekee hadi August Tanzania imepokea watalii wa kimataifa million mbili ambao wameingizia nchi dola za kimarekani million 3.5 hivyo kuzinduliwa kwa NMB QR PAY BY LINK inakuja kutoa suluhisho kubwa la malipo kwa wafanyabiashara na wateja wao wakiwemo watalii ambao wamekuwa wakitembea na lundo la kadi za kimataifa kwaajili ya kufanya malipo.
Kwa upande wao benki ya NMB, benki ambayo imeshinda tuzo ya kimataifa ya benki bora nchini mara kumi na moja mfululizo, wanasema kwa kutumia NMB QR PAY BY LINK, licha ya kuleta urahisi kwa wafanyabiashara na wateja wao, itaondoa kabisa gharama manunuzi ya mashine ya malipo POS ambayo wafanyabiashara walikuwa wananunua kwa dola za kimarekani kati ya mia tatu hadi mia tano huku kukiwa hakuna makato yoyote kwa fedha inayoingia kwenye akaunti ya mfanyabiashara.
Benki ya NMB inawahamasisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa nchini kutembelea matawi ya benki ya NMB kuweza kujisajili na kupata huduma hiyo, ambayo licha ya kuwarahisishia kwenye biashara zao, itawasaidia pia kutunza rekodi za kibenki ambazo zitawasaidia kupata mikopo kupitia benki ya NMB, benki ambayo kwa sasa inawateja zaidi ya million nane.
#NTTupdates