Na Mwandishi wetu.
Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally, ametangaza rasmi kuwa tarehe 3/8/2024 ndiyo siku ya kuadhimisha Simba day.
Simba day ni siku maalum kwa klabu hiyo kufanya tamasha kubwa likiongozwa na burudani mbalimbali, utambulisho wa wachezaji wapya na mwishoni mechi ya kirafiki.
Taarifa za awali zilieleza kuwa huenda kilele cha Simba day, Simba SC watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda.
#NTTupdates