×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA.

Spika Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia Leo huko Jijini Dodoma. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson, Katika ukurasa rasmi wa Bunge la Tanzania, ametangaza kutokea Kwa kifo cha Spika huyo Mstaafu. Ndugai amefariki dunia leo, Jumanne ya tarehe 06 Agosti, 2025.

“Kwa masikitiko makubwa naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu, Mheshimiwa Job Ndugai, kilichotokea leo Jijini Dodoma,” amesema Dkt. Tulia Ackson.

#NTTUpdates