×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TUME YA HAKI JINAI IMEANZA KUZAA MATUNDA

Wizara ya Maliasili na Utalii imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Jeshi la Polisi Tanzania katika maeneo ya Mafunzo na Oparesheni kwa Jeshi la Uhifadhi ikiwa ni utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai Nchini iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2023.

Aidha, katika makubaliano hayo Kaimu Katibu Mkuu CP Benedict Wakulyamba mbele ya Kamishna wa Operseheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi aliyemwakilisha Mkuu wa Polisi Haji Awadhi alieleza kuwa, mafunzo na oparesheni zitakazokuwa zinafanyika zitazingatia weledi, Haki za Binadamu na Utawala kutokana na hati iliyosainiwa leo.

Naye Kamishia wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadh Juma Haji alisema kuwa, Jeshi la Polisi liko tayari kwa ushirikiano wa vyombo hivi viwili, kwa kuwa kwao itakuwa fursa ya kujifunza masuala ya uhifadhi wa maliasili ili kuleta tija katika kushughulikia masuala ya uhifadhi unaozingatia haki za binadamu.

Utiaji saini wa Hati ya Makubaliano umefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii Swagaswaga Jijini Dodoma leo tarehe 06 Agosti 2025.