Na Mwandishi wetu.
Thailand ni miongoni mwa Taifa lililopatwa na madhara ya tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 lililotokea siku ya Ijumaa Machi 28, 2025 ambapo taarifa rasmi imetolewa kuwa zaidi ya watu 11 wamefariki Dunia huku mamia hawajulikani walipo.
Miongoni mwa mamia ambao hawajulikani walipo ni Wajenzi zaidi ya 100 waliokuwa wakijenga ghorofa lililoporoma jijini Bangkok.
Juhudi za kuwatafuta wengine ambao hawajulikani walipo zinaendelea huku wananchi wakitakiwa kuwa na utulivu wakati mamlaka zikiendelea na uwokoaji.
Tetemeko hilo la ardhi limepita kwenye mataifa mengine kama Myanmar ambapo Maelfu wamepoteza maisha, India, Bangladesh, Loas, na China.
#NTTupdates