Na Mwandishi wetu.
Wajumbe wa Baraza la Kata la ardhi wamepatiwa mafunzo ya mwongozo wa usuluhishi wa migogoro ya Ardhi kwa lengo la kutatua na kuleta ufumbuzi wa migogoro hiyo.
Mafunzo hayo yametolewa hii leo Juni 13, 2025 na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wakili Msomi wa Halmashauri ya Mji Babati Bw.Gwandumi Mwambage kwa wajumbe kutoka kata zote nane za Halmashauri ya Mji wa Babati.
Bw.Gwandumi amesema kuwa wajumbe wa Baraza la Kata kuwa ni wasuluhishi tu migogoro inayokuwa imetokea ila sio watoa hukumu kulingana na mwongozo wa sasa wa Baraza la Kata inayoelekeza katika utendaji wao wa kazi.
Sambamba na hilo amesisitiza wajumbe kuhakikisha wanatumia mwongozo wa usuluhishi wa migogoro ya Ardhi katika mabaraza ya Kata muda wote kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kutokuingiliana kimajukumu.
#NTTupdates.