
Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watoto wenye ualbino kushindwa kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu katika Halmashauri za Sengerema na Buchosa mkoani Mwanza Afisa Elimu Elimu maalum mkoani humo ameliomba shirika la action Aid kuisaidia jamii hiyo kwakushirikiana na Serikali ili kuhakikisha Watoto hao wanapata elimu
Akizungumza mara baada ya Hafla fupi ya kuhitimisha mradi wa Kesho Angavu kwa Watoto wenye ualbino uliokuwa ukitekelezwa katika wilaya za Kwimba na Misungwi na Shirika hilo Afisa elimu elimu maalum mkoani humo Meshack Masanja amesema mradi huo umefanya vizuri katika kuwasaidia Watoto wenye ualbino kwenye sekta ya elimu na afya hivyo ni vyema utakapoanza tena uangazie Buchosa na Sengerema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino mkoani Mwanza Tas Masumbuko Marko ameeleza mafanikio makubwa waliyoyapa kupitia mradi huo ikiwemo kutatua changamoto katika sekta ya afya elimu na Miundombinu ya Chama hicho
Akizungumzia mambo mbali mbali yaliyotekelezwa na mradi huo kwa muda wa mwaka mmoja Mchagizi kutoka shirika la Actioni Aid Yusuph Mbwambo amesema mradi umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwasaidi watu wenye ualbino katika nyanja tofauti tofauti ikiwemo kuwawezesha kiuchumi ambapo kwasasa mradi huo umefikia mwisho
Nae mmoja wa wanufaika wa mradi huo Hellen Ngilo amelishukuru shirika la Action Aid kwa kuwasaidia mambo mbali mbali huku akiliomba kuendelea kuwashika mkono pindi watakapoanzisha mradi mwingine
