
Na Mwandishi wetu.
Maduka 17 na Mali za stoo ambazo zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo June 11 katika eneo la Soko la Buseresere Wilaya ya Chato Mkoani Geita huku chanzo chake kikiwa bado hakijajulikana mara moja.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Mrakibu Mwandamizi Hamisi Dawa, amesema walipata taarifa ya tukio hilo majira ya saa 3:34 usiku na hadi Sasa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha moto.
Hamisi alibainisha kuwa walichelewa kufika eneo la tukio kwasababu walichelewa kupata taarifa ya tukio hilo Kwani kutoka kituo Cha Jeshi hilo adi eneo la tukio hilo ni takribani dakika 40 na walianza kuzima moto huo majira ya saa tatu usiku adi saa tisa alfajiri.
Ameongeza kuwa wanaendelea kuzungumza na wafanyabiashara ili kubaini athari iliyotokea pamoja na kufanya tathmini ya mali zilizoteketezwa na moto huo.
Amewataka Wananchi wote kwa ujumla kutumia namba kutoa taarifa za matukio ya moto pale yanaponitokeza na kutumia kwa kupiga namba ya dharura ya 114 ya jeshi hilo pale tu tukio la moto linapojitokeza ili kudhibiti matukio kwa haraka.
#NTTUpdaes