Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillius Wambura, ameeleza kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha unafanyika Kwa Amani na utulivu.
Akiwa Jijini Dar es salaam wakati wa kufunga kozi ya maofisa na wakaguzi wasaidizi Wa Polisi Waliomaliza Mafunzo Yao Katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Kurasini, IGP Wambura amesema Jeshi hilo halitamvumilia Mtu yeyote atakayevuruga Hali ya Amani na utulivu Katika kipindi chote Cha uchaguzi.
#NTTUpdates