×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KASI NDOGO YA UJENZI SOKO LA SAMAKI MKUYUNI YAWATIA WASIWASI VIONGOZI

Kamati ya Fedha na Uongozi ya Wilaya ya Nyamagana imeonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa soko la samaki Mkuyuni, ikimtaka mkandarasi kuongeza juhudi ili kukamilisha mradi huo ifikapo Julai mwaka huu.

Ziara ya kamati hiyo ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo soko hilo limebainika kuwa na changamoto za utekelezaji.

Wajumbe wa kamati wamesema kusuasua kwa mradi kunazua sintofahamu juu ya hatma yake, wakisisitiza uwajibikaji na usimamizi madhubuti.

Akizungumza kwa upande wake, Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constentine Sima, amesema hakutakuwa na nyongeza ya muda kwa mkandarasi endapo hatakamilisha mradi kwa wakati uliopangwa.

NTTUPDATES.