×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC SENDINGA AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO SIMANJIRO.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga, amefanya uzinduzi mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro.

Mnara huo uliogharimu zaidi ya milioni 200 mpaka kukamilika unatarajiwa kuhudumia wananchi wa kijiji cha Kimotorok na vijiji jirani, Sendiga amesema Serikali ya awamu ya sita imeendelea na juhudi za kuhakikisha wananchi wa maeneo ya pembezoni na vijijini wanapata mawasiliano ya uhakika Kwa kujenga minara ya mawasiliano kupitia mfuko wa mawasiliano Kwa wote (UCSAF).

Pia, ametembelea na kukagua zahanati ya Oltotoi, ujenzi wa mradi wa maji Oltotoi awamu II na kukabidhi vifaa kwaajili ya ujenzi wa mradi huo utakao gharimu shilingi milioni 297.537. sambamba na hilo ametembelea Kijiji cha Loiborsiret kwenye eneo mwekezaji la IRALOI RANCHING ambao wanajishughulisha na shughuli za utalii .

RC Sendiga anatarajiwa kuhitimisha ziara yake hii leo Mei 7. 2026 kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Loiborsiret.

NTTupdates.