
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 17, 2026 amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo mkoani Arusha ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027 itakayofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu yote muhimu kwa ajili ya mashindano hayo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa kimataifa. Amesema ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuendelea kuimarisha sekta ya michezo pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi kupitia mashindano makubwa ya kimataifa.
Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutasaidia kukuza vipaji vya michezo, kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kuchochea shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani. Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha maandalizi ya AFCON 2027 yanafanikiwa na kuiacha Tanzania katika nafasi nzuri ya kunufaika na mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

NTTUPDATES
