×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

IDADI YA VIFO HANANG’ YASALIA 89 ASEMA MOBHARE MATINYI.

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi amesema kuwa Serikali inaendelea kuwaunganisha waathirika wa mafuriko ya Hanang’ na familia zao ambapo hadi sasa imefanikiwa kuwarejesha kwa ndugu zao waathirika 460 wanaotoka katika kaya 133.

Matinyi ameyasema hayo leo Disemba 15, 2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hadi sasa idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko yaliotokea kijiji cha Gendabi Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara haijaongezeka imebaki kuwa 89 huku majeruhi waliobaki katika hospitali za Mkoa huo wakiwa ni 14.

Amesema kuwa Serikali inahakikisha kila kaya inayoondoka inapewa chakula cha kutosha na mahitaji ya siku 30 na vitu muhimu wanavyovihitaji ili kuanza maisha yao.

#NttUpdates