×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAKUNDI MAALUM MWANZA YAPEWA ELIMU NA KUSAJILIWA NeST KUNUFAIKA NA ZABUNI ZA SERIKALI.

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza imetoa elimu na kufanya zoezi la usajili kwa makundi maalum kuhusu matumizi ya mfumo wa NeST, ili kuyawezesha kunufaika na fursa za zabuni za Serikali.

Akizungumza leo katika ukumbi wa Gand Hall, Afisa wa PPRA Kanda ya Ziwa, Mhe. Josephat Mafugulu amesma Serikali imeweka msisitizo kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 pamoja na kanuni zake za mwaka 2024, kwamba kila taasisi nunuzi inatakiwa kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake kwa ajili ya makundi maalum.

Aidha ameongeza kuwa makundi hayo yanajumuisha wanawake, vijana, wazee pamoja na watu wenye ulemavu.

Pia ameongeza kuwa zoezi la usajili kwenye mfumo wa NeST linalenga kuyawezesha makundi hayo kushiriki kikamilifu katika zabuni zinazotengwa mahsusi kwa ajili yao.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Michael Simon Magesa, amesma elimu iliyotolewa inalenga kuyajengea uwezo makundi hayo ili yaweze kujisajili na kushiriki ipasavyo kwenye mfumo huo.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza halmashauri ya jiji la mwanza kwa kuwapatia mafunzo hayo kwa imewasaidia kuunda vikundi na kupata mkopo huo unaotolewa na halmashauri hiyo .

NTTUPDATES.