
JESHI la polisi Mkoani Geita limedhibitisha tukio la kuuwawa kwa mfanyabiashara wa vifaa vya pikipiki aliefahamika kwa jina Alex Mayaya mwenye umri wa miaka (40) kwa kupigwa na walinzi dukani kwake waliodhania kuwa ni mwizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo na kueleza tukio lilitokea usiku wa kuamkia siku ya jumatatu ya Novemba 6, 2023.
Mfanyabiashara huyo ambae Kwa Sasa ni marehemu alikuwa ni shabiki wa timu ya Yanga na baada ya ushindi wa timu hiyo dhidi ya watani zao Simba marehemu huyo anadaiwa alishangilia kwa kulewa na marafiki na kisha akarejea dukani kwake na ndipo umauti ulimkuta akiwa huko.
“Alipofika dukani kwakwe walinzi hawamfahamu vizuri kwa hiyo wakahisi ni mwizi kwa hiyo baada ya kuhisi ni mwizi walimkamata na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na rungu.”
Kamanda Jongo amesema kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa walinzi wale kiligusa eneo la mshipa mkubwa wa damu hali iliyopelekea maumivu makali kwa mfanyabiashara na ilipofika asubuhi ya Novemba 6, 2023 ikapelekea kifo chake.“
Kulipokucha wananchi wanaomfahamu wakagundua yule siyo mwizi, isipokuwa ni mwenyeduka, kwa hiyo wakampeleka kituoni akapewa PF3, lakini alipofikishwa hospitali alifariki muda mfupi baadaye.”
#NTTUpdates