Watu watatu akiwemo na mganga wa kienyeji aitwaye Ezekiel Charles wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya mwanamke aliyejuliakana kwa jina la Esther Lukonu mwenye umri wa miaka 51 wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.
Washtakiwa waliofikishwa mahakamani ni pamoja na Masunga Mabula mwenye umri wa miaka 32, Ezekiel Charles mwenye umri wa miaka 40 ambae ni mganga wa kienyeji pamoja na Salome Raphael mwenye umri wa miaka 32, ambao wawsomewa kesi namba sita ya mwaka huu mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Amani Mahimba wa mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
Akiwasomea shtaka la mauaji linalowakabili mwendesha mashtaka wa serikali mkaguzi msaidizi wa polisi Chacha Msenye amesema mnamo tarehe kumi ya mwezi watano mwaka huu washtakiwa hao wanadaiwa kumuuwa mwanamke aitwaye Esther Lukoni kwa kumnyonga shingo kisha wakambaka na kumkata sehemu zake za siri na mwili wake wakautupa kwenye shamba la mihogo.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shtaka hilo la mauaji na kupelekwa rumande katika gereza la wilaya ya magu hadi tarehe 16 ya mwezi huu kesi hiyo itakapotajwa tena.