×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TIGO TANZANIA YATAJWA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA

Na Mwandishi wetu.

IMEELEZWA kuwa Mtandao wa kampuni ya Tigo Tanzania ni moja kati ya mitandao inayokuwa kwa kasi hali inayorahisisha njia za mawasiliano na kuchangia kuboresha maisha ya watanzania.

Hayo yamesemwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni hiyo Isaac Nchunda leo Agosti mosi 2024 katika ofisi za Tigo jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa katika kuhakikisha kampuni ya Tigo inaendelea kurahisisha maisha , imepeleka kampeni ya SakoKwaBako ambayo sasa ina miezi miwili tangu ianzishwe.

“Leo tigo ipo kanda ya kati na tumewaletea kampeni ya SakoKwaBako ambayo sasa ina miezi miwili, ikiwa Kanda ya kati Dodoma Makao Makuu ya nchi na ni siku nzuri ambayo usafiri wa reli ya mwendokasi (SGR) imezinduliwa ,tigo ndiyo mtandao bora zaidi Tanzania kwa sababu tuna teknolojia ya karne ya hivi sasa ya 4G na 5G,

“Na hapa Dodoma tunayo 5G hivyo tunatoa huduma nzuri kwa wateja wanaotumia mtandao wa Tigo ambapo wanafurahia huduma yenye kasi zaidi ya 5G.”amesema Isaac

Amesema SakoKwaBako inatoa bonasi kwa kila mteja anayenunua bando la tigo anapata MB na dakika za bure.

Amewaasa wananchi wajiunge zaidi na mtandao huo ili wanaufaike na ofa hizo ambapo pia ameizungumzia kampeni yao kupitia simu aina ya ZTE A34 ambapo amesema hiyo ni simu ya kisasa ZTE kupitia simu ya kisasa zaidi na inapatika kwa unafuu zaidi.

“Simu hii inauzwa shilingi 180,000 lakini pia inatolewa kwa mkopo ambapo mteja atatanguliza kiwango cha awali cha sh.35,000 na sh650 kwa siku hadi mteja atakapomaliza deni lake na wakati huo huo wanaendelea kutumia simu yake kabla hata ya kumaliza deni lake.”amesisitiza

Akizungumzia kuhusu huduma za tigo kwa ujumla kampuni hiyo unahudumia wateja zaidi ya milioni 21 huku akisema hiyo ni kwa sababu ya ubora wake.

“Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na kwamba Tigo ndiyo mtandao unaijua kwa kasi zaidi nchini. “Amesema

#NTTupdates