×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WAFANYABIASHARA DODOMA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.
Washiriki wa kikao hicho.


Na mwandishi wetu,Dodoma


WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa zinazojitokeza kwa kujenga miundombinu wezeshi kwa wawekezaji na wageni kwani baada ya Serikali kuhamia jijini Dodoma kumekuwa na ongezeko la wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kijaji ameyasema hayo Agosti 17, 2023 wakati wa kikao kazi na wafanyabiashara wa Jiji la Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jengo la Mkapa ambapo kikao hicho kimewahusisha wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali.

Waziri Kijaji amesema uchumi imara wa Taifa upo mikononi mwa sekta binafsi hivyo amewahimiza wafanyabiashara hao kutumia fursa zote zinazojitokeza iwe ni sekta binafsi au kutoka serikalini ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.


Waziri Kijaji amewahimiza wajasiriamali kuwa waaminifu na fedha zinazotolewa na Serikali kama sehemu ya mtaji ili kuwawezesha na wengine kupata fursa hiyo.

“Lazima tukubaliane na utaratibu uliowekwa uadilifu wetu, uaminifu wetu ni muhimu hakuna fedha za bure sehemu yeyote lazima uwe na uhakika wa fedha kurudi na mtu unae mpatia fedha hivyo tunatakiwa kumthibitishia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama alivyo mtetezi wetu namba moja “ameeleza Kijaji

Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa salamu za Mkoa amempongeza Waziri huyo kwa kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na kutatua changamoto na kero zilizokuwa kikwazo katika utekelezaji wa biashara zao.

Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma upo tayari kupokea wawekezaji na kuongeza idadi ya viwanda ili kuongeza na kukuza mapato ya Serikali na uchumi wa nchi ya Tanzania.

Mwisho.