

-Miradi yote yapitishwa na Mwenge wa Uhuru 2026 hakuna mradi uliokataliwa.
Mwenge wa Uhuru umeendelea kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo April 15, 2026 umekimbizwa Wilaya ya Temeke ikiwa ni Wilaya ya tatu kikimbiza mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo.
Mwenge wa Uhuru katika wilaya hiyo umepitia miradi nane yenya thamani ya Tsh 13,664,218,741 ambayo ni Mradi wa uwekezaji wa Kiuchumi Home City Kata ya Chang’ombe, ujenzi wa barabara ya Mwakalinga yenye urefu wa Km 1.07 kata ya chang’ombe, mradi wa huduma ya watoto wachanga umri wa siku 0-28 kituo cha Afya Yombo vituka.

Vilevile mradi wa uchimbaji na usambazaji wa maji kata ya Makangarawe, ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Toangoma, ujenzi wa ghorofa 4 shule ya sekondari kibonde maji, mradi wa uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa na mwisho mradi wa kufyatua matofali (Fevmaz Hero Group) kata ya Chamazi.
Aidha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 16, 2026 unaendelea kukimbizwa katika Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo utakagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo

