Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Ufaransa Hugo Ekitike (23) atakosa michezo iliyosaloa ya ligi kuu ya uingereza (EPL) na michuano mikubwa ya soka ya kombe la Dunia 2026 na mechi ambalo linatarajiwa kufanyika kwenye mataifa matatu ya Marekani, Mexico na Canada.
Ekitike ambaye aliumia hapo jana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya kati ya Liverpool dhidi ya PSG uliopigwa dimba la Anfield na timu yake ikalazimishwa kichapo cha magoli 2-0.
Ekitike atalazimika kukaa nje kwa zaidi ya miezi 8 hadi 9 kuuguza jeraha lake la kamba ya kisigino (Achilles Tendon).

Msimu huu Ekitike amecheza jumla ya michezo 28, akifunga magoli 11 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli (assist) 5.