
Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Al Qadsiah inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League), imemtambulisha mshambuliaji wao mpya Mateo Retegui mwenye umri wa miaka 26 akitokea klabu ya Atalanta ya (serie A) Italia.
Al Qadsiah imemsajili Retegui kwa dau la Euro Milioni 65 huku ikimpatia nyota huyo mkataba wa miaka mitatu ambapo amechukua mikoba ya mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre Emerick Aubameyang ambaye amevunja mkataba na klabu hiyo.
#NTTupdates