×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

UBAYA UBWELA MNYAMA ATINGA NUSU FAINALI CAFCC

Na Mwandishi wetu.

Historia imeandikwa na uteja umeisha kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam baada ya mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), umemalizika kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya Al Masry huku Mnyama akitinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kupitia mikwaju ya penati 4-1.

Mchezo huo ulishuhudia Mlinda mlango namba moja wa Simba SC Moussa Camara akifanikiwa kucheza mikwaju miwili ya penati na kupeleka furaha baada ya kufuzu hatua hiyo.

Simba SC imefanikiwa kufuzu nusu fainali yao ya kwanza ya kombe la shirikisho Afrika CAFCC baada ya kucheza zaidi ya mara 6 hatua hiyo kwenye michuano mikubwa ya Afrika ya vilabu na kushindwa kufuzu.

#NTTupdates